Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2018

SOMO # 03: MAAJABU YA NAMBA SABA

 MAAJABU YA NAMBA SABA (7) Mungu ni wa ajabu Sana hakika hakuna mwanadamu awezaye kumchunguza maaana Yeye ndiye mwenye siri kubwa wa hii namba 7 katika ulimwengu wa ki-Roho. Mpendwa tunapoenda kuumalizia huu mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019 naomba tuone haya maajabu makubwa ya namba 7 ambayo Mungu ndio anaijua Siri yake. Na haya maajabu ya namba Saba ninayoenda kuyaandika si kwamba ni yote ila ni kwa uwezo wa kufikiri kwangu na kusoma Biblia vile vile pamoja na Roho Mtakatifu kunipa mzigo wa kuandika somo hili maana nimeanza kuliandaa kwa muda mrefu kidogo. Mpendwa nakujulisha kuwa hili somo ni refu hivyo basi Mungu akusaidie usome kwa umakini pasipo kuishia njiani ili uweze kumaliza. _Mambo hayo ni Kama yafuatayo;-_ 1. Mungu ana Roho 7. UFUNUO 4:5 imeandikwa;- Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti ya ngurumo na taa Saba za Moto zikiwaka  mbele ya kile kiti cha enzi ndizo Roho Saba za Mungu. 2. Kitabu kilicho Mbinguni kina Mihuri 7. UF...