SOMO # 03: MAAJABU YA NAMBA SABA


 MAAJABU YA NAMBA SABA (7)

Mungu ni wa ajabu Sana hakika hakuna mwanadamu awezaye kumchunguza maaana Yeye ndiye mwenye siri kubwa wa hii namba 7 katika ulimwengu wa ki-Roho.

Mpendwa tunapoenda kuumalizia huu mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019 naomba tuone haya maajabu makubwa ya namba 7 ambayo Mungu ndio anaijua Siri yake.

Na haya maajabu ya namba Saba ninayoenda kuyaandika si kwamba ni yote ila ni kwa uwezo wa kufikiri kwangu na kusoma Biblia vile vile pamoja na Roho Mtakatifu kunipa mzigo wa kuandika somo hili maana nimeanza kuliandaa kwa muda mrefu kidogo.

Mpendwa nakujulisha kuwa hili somo ni refu hivyo basi Mungu akusaidie usome kwa umakini pasipo kuishia njiani ili uweze kumaliza.


_Mambo hayo ni Kama yafuatayo;-_


1. Mungu ana Roho 7.

UFUNUO 4:5 imeandikwa;- Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti ya ngurumo na taa Saba za Moto zikiwaka  mbele ya kile kiti cha enzi ndizo Roho Saba za Mungu.


2. Kitabu kilicho Mbinguni kina Mihuri 7.

UFUNUO 5:1 imeandikwa;- Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake Yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma kumetiwa Mihuri 7


3. Mungu alimaliza kazi siku ya 7, akaibariki siku ya 7 , akastarehe na hakufanya kazi siku ya 7.

MWANZO 2:2-3 imeandikwa;-
2. Na siku ya Saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya akastarehe siku ya Saba akaacha kufanya kazi yote aliyoifanya.
3. Mungu akaibariki siku ya Saba akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.


4. Mungu alimuagiza NUHU awaingize wanyama safi Saba(7)  Saba(7) mume na mke pia na ndege Saba Saba mume na mke katika ile safisa kabla ya gharika kuanza.

MWANZO 7: 2'a'-3 imeandikwa;-
2'a'. Katika wanyama wote walio safi ujitwalie Saba Saba mume na mke.
3. Tena katika ndege wa angani Saba Saba mume na mke ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote.


5. Malaika mkuu MIKAELI ana herufi 7.

Huyu ni mkuu wa malaika wote huko juu Mbinguni, yaani yeye ndio kiongozi mkuu wa malaika Wengine wote ,miongoni mwa malaika ambao huongozwa na Malaika mkuu ni Malaika GABRIELI.

YUDA 1:9 imeandikwa;-
Lakini Mikaeli Malaika mkuu aliposhindana na ibilisi na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu bali alisema Bwana na akukemee.


6. Neno MALAIKA,IBILISI na SHETANI lina herufi 7.

UFUNUO 12:7-9 imeandikwa;-
7. Kulikuwa na Vita Mbinguni Mikaeli na Malaika zake wakapigana na yule joka,yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake.
8. Wao hawakushinda Wala mahali pao hapakuonekana tena Mbinguni
9. Yule joka akatupwa,yule mkubwa nyoka wa zamani aitwae Ibilisi na Shetani audanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

Kumbe:
Shetani ana malaika zake
Mungu ana Malaika zake.

Hivyo basi tunapokuwa kwenye maombi kila siku tumuombe Mungu amsambalatishe Shetani na malaika zake katika maisha yetu.


7. Neno MSALABA lina herufi 7.

Mpendwa msalaba ndio mkombozi wetu sisi wanadamu ambapo Yesu Kristo ndio aliteswa na kutufia pale ili kuweza kuukomboa ulimwengu wote.

WAKOLOSAI 1:20 imeandikwa;-
Na kwa Yeye huvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya Imani kwa damu ya Msalaba wake kwa Yeye ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi au vilivyo Mbinguni.


8. Neno HEZEKIA lina herufi 7

Huyu ni Mfalme ambaye alikuwa akiumwa Sana kwahiyo Mungu alimwambia nabii Isaya aende kumweleza kuwa atengeneze nyumbani kwake maana anaenda kufa,basi baada ya nabii Isaya kumpa hizo taarifa Mfalme Hezekia alimliliya Mungu Sana asimchukue yaani asife

Mungu alisikia kilio Cha Mfalme na akamwambia tena nabii Isaya aende kumweleza Mfalme Hezekia kuwa hata kufa tena bali amemuongezea mbele Miaka 15 na kumpa ulinzi zidi ya maadui.

Kasome 2 WAFALME 20:1-6 ni habari ndefu ndio maana nimeacha kuinukuu.


9. Lile Joka jekundu  lililotupwa hapa duniani kutoka Mbinguni lina VICHWA 7 na VILEMBA 7.

UFUNUO 12:3 imeandikwa;-
Ikaonekana ishara nyingine Mbinguni na tazama Joka kubwa  jekundu alikuwa na Vichwa Saba na pembe kumi na juu ya Vichwa vyake Vilemba Saba .


10. Henoko ni mtu wa 7 baada ya Adamu.

YUDA 1:14 imeandikwa;-
Na Henoko mtu wa Saba baada ya Adamu alitoa maneno ya unabii juu ya hao akisema angaliya Bwana alikuja na watakatifu wake maelfu maelfu.


11. Daudi alikuwa anamsifu Mungu Mara 7 kwa siku.

ZABURI 119:164 imeandikwa;-
Mara Saba kila siku nakusifu kwa sababu ya hukumu za haki yako.


12. Wafilisti walikaa na Sanduku la Mungu yaani la Agano kwa muda wa miezi 7.

Sanduku hili la Bwana waliwapora na kuwauwa watoto wa mtumishi Eli ambao ni Finehasi na Hofni  ndio walikuwa nalo wakilitunza baada ya kupewa kutoka kwa baba yao.

1 SAMWELI 6:1 imeandikwa;-
Basi hilo sanduku la Bwana lilikuwamo katika nchi ya Wafilisti muda wa miezi Saba


13. Mikate 7 ililiwa na watu elfu nne baada ya Yesu Kristo kutenda miujiza.

MATHAYO 15:36 imeandikwa;-
Akaitwaa ile Mikate Saba na vile visamaki akashukuru akavimega akawapa wanafunzi wake nao wanafunzi wakawapa makutano.

MATHAYO 16:10 imeandikwa;-
Wala ile Mikate Saba kwa watu elfu nne na makanda mangapi mliyoyaokota?

14. Dunia ina Mabara 7
15. Wiki moja ina siku 7
16. Tarehe 7 mwezi wa 7 kila mwaka huwa ni sikukuu ya Wafanyabiashara na ni siku ya Mapumziko.

Mpendwa ubarikiwe Sana naamini umejua baadhi ya Mambo ambayo ulikuwa huyafahamu kuhusu namba Saba japo Siri ndio anaijua Mungu.

AMANI YA BWANA WETU YESU  KRISTO IWE PAMOJA NASI.


©Msufu Dec,  2018.

 

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO # 01: ADUI

SOMO # 07: MAOMBI