Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2019

SOMO # 07: MAOMBI

MAOMBI Utangulizi: Maombi ni mawasiliano kati ya Muombaji na Mungu , Maombi kwa sisi wacha Mungu hayaepukiki maana tukikaa kimya na kusema unampenda Mungu bila Maombi na kusoma Neno ni rahisi Sana kurudi nyuma kiimani maana adui atatushambulia kirahisi mnooo. Na majaribu yatatushambulia mengi mnooo katika maisha yetu na tutashindwa kuyaepuka kwa sababu hatudumu katika maombi. Baadhi ya watu wengi wamekuwa na mzigo yaani shauku ya maombi pale wanapopata shida Mfano mtu anamuomba Mungu ampe kazi yaani apate ajira, aolewe yaani apate mume, aowe yaani apate mke, apate biashara ya kufanya,apate gari,apate fedha,apate safari labda ya kwenda nje ya nchi au anaumwa ugojwa fulani n.k ndio utamwona yapo bize na Mungu na kanisani haachi kuhudhuria kila Jumapili na hata kwenye zile ibada za katikati ya wiki hakosi Lakini akisha kipata kile anachokihitaji kutoka kwa Mungu kupitia yale Maombi aliyokuwa akiyaomba kila siku, utamwona Maombi amepunguza kabisaaa na hat...