SOMO # 07: MAOMBI

MAOMBI


Utangulizi:
Maombi ni mawasiliano kati ya Muombaji na Mungu , Maombi kwa sisi wacha Mungu hayaepukiki maana tukikaa kimya na kusema unampenda Mungu bila Maombi na kusoma Neno ni rahisi Sana kurudi nyuma kiimani maana adui atatushambulia kirahisi mnooo. Na majaribu yatatushambulia mengi mnooo katika maisha yetu na tutashindwa kuyaepuka kwa sababu hatudumu katika maombi.

Baadhi ya watu wengi wamekuwa na mzigo yaani shauku ya maombi pale wanapopata shida Mfano mtu anamuomba Mungu ampe kazi yaani apate ajira, aolewe yaani apate mume, aowe yaani apate mke, apate biashara ya kufanya,apate gari,apate fedha,apate safari labda ya kwenda nje ya nchi au anaumwa ugojwa fulani n.k ndio utamwona yapo bize na Mungu na kanisani haachi kuhudhuria kila Jumapili na hata kwenye zile ibada za katikati ya wiki hakosi

Lakini akisha kipata kile anachokihitaji kutoka kwa Mungu kupitia yale Maombi aliyokuwa akiyaomba kila siku, utamwona Maombi amepunguza kabisaaa na hata kuhudhuria kwenye Ibada kunakuwa kumepungua kwa kiasi kikubwa Sana pasipo kujua kwamba kile ulichokuwa unakiomba na Mungu akakupatia ndio inatakiwa uzidishe maombi kila siku kukiombea ili shetani asije akakupokonya, kutokuomba ndio kuna sababisha majaribu kuwa Mengi juu ya hicho kitu ulichopewa kwa sababu umeacha kuomba baada ya kupata.

Ndiyo maana unaweza kuta watu migogoro kwenye ndoa haiishi kila kukicha kwa sababu mwenye msingi wa hiyo ndoa mmemwacha baada ya kuwa mmeoana ( na maanisha maombi mmeyaacha baada ya kuoana) , au unakuta watu migogoro haishi huko kwenye kazi walipoajiriwa au kwenye biashara ni kwa sababu wameacha kuomba kabisa baada ya kuwa wamepatiwa na Mungu wakizan kuwa safari ya maombi ndio imeishia hapo.

Maombi hayana mipaka Wala hayana ukomo mpaka ifikie hatua ya kusema nimeomba vya kutosha sasa inatakiwa nipumzike kufanya maombi Kama wiki mbili hivi au mwaka au mwezi n.k , ukifanya hivyo unakuwa umeenda kinyume na Neno la Mungu maana kwenye Biblia 1 WATHESALONIKE 5: 17 imeandikwa;- Ombeni bila kukoma.

Kwahiyo maana yake ni kwamba Maombi ni chakula cha ki roho Kama ilivyo mwili huulisha kila siku na Roho inatakiwa kuilisha kila siku maombi ili shetani asije pata nafasi ya kuivuruga roho yako mpaka akarudishe nyuma kiimani kwa kumfata yeye.

Tumwombe Mungu kila siku pasipo kuchoka haijalishi tuna shida au hatuna shida maana maombi tuyaombayo kila siku tusizani yanapotea bure bure ,hapana Mungu anayaweka akiba na yanakuja kutumika pale ambapo Mungu anaona inafaa kwa wakati wake yaani kwenye hitaji au changamoto fulani.

Katika maombi tunayo mwomba Mungu kupitia jina tulilopewa la Yesu Kristo , si yote yanajibiwa Kama tulivyoomba KWASABABU Mungu hujibu maombi yaliyo sawasawa na mapenzi yake maana Yeye ndio anatujua sisi vizuri kabisa kuliko sisi tunavyojijua.

Mungu kabla hajatujibu kile tunachokiombea huwa Kuna baadhi ya Mambo anaya fikiria Kwanza kabla hajatupatia.

Biblia inaposema kwenye MATHAYO 7:7 kwamba;- Ombeni nanyi mtapewa,tafuteni nanyi mtapata,bisheni mlango nanyi mtafunguliwa.

Haimaanishi kwamba kila utakachokiomba utapewa na Mungu kama ilivyoandikwa kwenye huo mstari hapo juu, kwa sababu Mungu kuna mambo Mengine anayatazama Kwanza zaidi ya hicho tunachokiomba kabla ya kujibu.

MATOKEO YA MAOMBI KUHUSU UNACHOKIOMBA.

Kama nilivyosema Mungu hujibu sawasawa na Mapenzi yake kwenye kila unachokiomba
Hivyo basi unapo omba ni lazima ujue mambo yafuatayo ya hicho unachokiombea yanaweza kutokea

1. Mungu anaweza kukujibu sawasawa na ulivyoomba.
2.Mungu anaweza kukujibu tofauti na ulichoomba.
3. Mungu anaweza kukujibu zaidi ya ulichoomba yaani akakuongezea mara dufu.
4. Mungu anaweza asikujibu kabisaaaaa kwa wakati uliupanga wewe au asijibu kabisa.

Kwahiyo ukishayajua hayo mambo manne hapo juu haitakupa shida na kuanza kulalamika kwa kusema mbona Mungu hanijibu wakati huwa namuomba kila siku?!
Mpendwa sababu zipo ni kwa Nini Mungu asikujibu kile unachokiombea au anakuja kujibu kitu tofauti kabisaaa , au anakujibu mara mbili zaidi ya ulichokuwa unataka au anachelewa kukupa kile ambacho unakitaka kwa wakati uliopanga wewe.

SABABABU ZA MUNGU KUFANYA HIVYO NI KAMA ZIFUATAZO;-

1. Wakati
Mungu huwa tunapoomba anaangalia je tunachokiomba kipo kwenye wakati na mpango wake??
Maana katika MHUBIRI 3:1 imeandikwa;- Kwa kila Jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya Mbingu.

Mungu huwa hachelewi Wala hawahi ,kwahiyo unaweza ukawa unaombea Jambo kwa muda mrefu Sana lakini Mungu akaja kujibu kwa wakati na majira yake, kinachotakiwa ni uvumilivu wa kusubiri na kuendelea kudumu katika maombi pasipo kuchoka hata kama atakujibu usichoke kuendelea kuomba.

Ndio maana katika LUKA 18:1 imeandikwa;- Akawambia Mfano ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala msikate tamaa.
Kwhyo tusikate tamaa kwa wakati na majira yake Mungu ndio atatujibu.

2. Imani.
Mungu kabla ya kujibu huwa anaangalia imani ya huyo mtu anayemwomba , kwahiyo imani yako ndio itaonesha ujibiwe au usijibiwe au ujibiwe baadaye au ujibiwe kwa muda unaotaka wewe au ujibiwe zaidi ya unachoomba.

Kwenye kitabu cha YAKOBO 1:6-8 imeandikwa;-
6. Ila na aombe kwa Imani pasipo shaka yoyote,maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku.
7.Maana mtu Kama yule asidhani yakuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8. Mtu wa nia mbili husita sita katika njia zake.

Kwahiyo unapoomba juu ya Jambo fulani usiwe na mashaka yoyote kwa kusema sijui Mungu anaweza jibu au hawezi? ukifanya hivyo Unakuwa unamkosea Mungu maana Mungu hashindwi na kitu chochote kwenye hii dunia , LUKA 1:37 imeandikwa;- Kwa kuwa hakuna neno lisiliwezekana kwa Mungu.

3. Nia ya mtu.
Mungu kabla hakajibu anaangalia Je! Nini nia ya hiki kitu anachoniomba?? Je! Anataka kukitumia vizuri au vibaya? Maana Kuna mtu mwingine anaomba Jambo fulani ili akipatiwa awe anajionesha kwa watu au awe anawanyanyasa wale hawana, yaani awe anajitapa mataani kuwa yeye ndio yeye hakuna mwingine zaidi yake, mambo yote hayo Mungu huwa anayaangalia ndani ya moyo wa mtu.
Ki uharisia unaweza ukaomba Jambo na usilipate kabisaaaaa kwa sababu nia ya moyo wako inaongozwa na tamaa mbaya juu ya hicho kitu ukikipata ndio maana katika YAKOBO 4:3 imeandikwa;- Hata mwaomba vibaya wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya ili mvitumie kwa tamaa zenu.
Tuache kuendeshwa na hisia za mwili na tamaa mbaya tunapokuwa tunaenda kwenye maombi kuhusu kuombea Jambo fulani, maana Mungu anaiangalia mioyo yetu inawaza Nini juu ya hilo Jambo tunalotaka kutendewa.

4. Maovu.
Kuwa na matendo mabaya ni moja ya sababu Mungu anaiangalia kabla hajajibu maombi, mtu anapotenda dhambi halafu anaenda kwenye maombi bila ya kuomba toba na rehema kuombea Jambo fulani hapo Mungu huwa anachukia Sana na hatimaye inasababisha asijibu kile unachokihitaji, na hata katika YOHANA 9:31imeandikwa;- Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi Bali mtu akiwa ni mcha Mungu na huyafanya Mapenzi yake humsikia huyo.

Pia katika MATHALI 28:9 imeandikwa;- Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria Hata sala yake ni chukizo.

Kwahiyo maombi ya wenye dhambi ni chukizo mbele za Bwana.
Mpendwa inatupasa tuwe watu wa toba kila muda maana tunamadhaifu mengi sana ambayo husababisha kumkosea Mungu na mpaka kupelekea asitujibu tunachokihitaji.

Ubarikiwe Sana mpendwa

AMANI YA BWANA WETU YESU KRISTO IWE PAMOJA NASI.

©Msufu Mrch, 2019

Maoni

  1. Nimebarikiwa Sana na ninaendelea kulifuatilia somo hili kwa kina zaidi

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO # 03: MAAJABU YA NAMBA SABA

SOMO # 01: ADUI