Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2021
  SOMO # 11:   MKARIBIE MUNGU NAYE ATAKUKARIBIA HUU MWAKA 2021 Yakobo 4:8 imeandikwa;- Mkaribieni Mungu naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi ,na kuisafisha mioyo yenu enyi wenye nia mbili. Mpendwa natumaini u mzima wa afya kabisa, na unaendelea vizuri na majukumu yako kama kawaida. Kabla sijaendelea naomba kukuuliza hili swali ndugu mpendwa unayesoma ujumbe huu. Je! Ni mambo ngani upo nayo karibu toka huu mwaka uanze?? Je! Ni Mazuri au Mabaya?? Mpendwa Mungu anatukumbusha siku hii ya leo tugeuke kwa kutoka kule ambapo tumekuwa karibu na Mambo mabaya ambayo yanatupekelea kubaya,   kwa sababu mambo hayo yataharibu maisha yetu kabisa. Ukiwa karibu na Mungu siku zote naye atakuwa karibu na wewe kwa kila jambo ambalo utakuwa unalitenda , utakalolihitaji na hata kwa mambo utakayoyapitia yawe mabaya au mazuri lazima Mungu atakuwa pamoja na wewe. Mpendwa usiwe karibu na dhambi , itakupeleka pabaya 1.    Usiwe karibu na Ulevi ,bali ...