SOMO # 11: MKARIBIE
MUNGU NAYE ATAKUKARIBIA HUU MWAKA 2021
Yakobo 4:8 imeandikwa;- Mkaribieni Mungu naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu enyi wenye
dhambi ,na kuisafisha mioyo yenu enyi wenye nia mbili.
Mpendwa
natumaini u mzima wa afya kabisa, na unaendelea vizuri na majukumu yako kama
kawaida.
Kabla
sijaendelea naomba kukuuliza hili swali ndugu mpendwa unayesoma ujumbe huu.
Je! Ni mambo ngani upo nayo karibu
toka huu mwaka uanze?? Je! Ni Mazuri au Mabaya??
Mpendwa
Mungu anatukumbusha siku hii ya leo tugeuke kwa kutoka kule ambapo tumekuwa karibu
na Mambo mabaya ambayo yanatupekelea kubaya, kwa sababu mambo hayo yataharibu maisha yetu
kabisa.
Ukiwa karibu
na Mungu siku zote naye atakuwa karibu na wewe kwa kila jambo ambalo utakuwa
unalitenda , utakalolihitaji na hata kwa mambo utakayoyapitia yawe mabaya au
mazuri lazima Mungu atakuwa pamoja na wewe.
Mpendwa
usiwe karibu na dhambi , itakupeleka pabaya
1. Usiwe karibu na Ulevi ,bali Kuwa
karibu na Mungu naye atafanya mambo makubwa katika maisha yako.
2. Usiwe karibu na Uzinzi maana utaishia
pabaya mpendwa, bali Kuwa karibu na Mungu naye atafanya mambo makubwa katika
maisha yako.
3. Usiwe karibu na marafiki wabaya maana
watakupeleka pabaya, bali Kuwa karibu na Mungu naye atafanya mambo makubwa
katika maisha yako.
4. Usiwe karibu na Wavivu huu mwaka
maana na wewe utaishia kuwa mvivu tuu ,hatimaye hutaweza kutimiza lengo lako
hata moja kwa huu mwaka.
5. Usiwe karibu na watu wenye kukatisha tamaa
,maana na wewe utakata tamaa kwa baadhi ya mambo uliyopanga kuyatekeleza huu
mwaka.
6. Usiwe karibu na watu matapeli,waongo,wafitinishaji,n.k
maana na wewe utaishia kuwa hivyo tu.
Mpendwa kuwa
karibu na Mungu maana yake ni kumwamini na kumtumikia Yeye, mpendwa hutajuta
hata siku moja kuwa ndani ya Yesu.
Kuwa ndani
ya Yesu kuna faida kubwa sana wala hakuna hasara yoyote, bali kuwa ndani ya
shetani hakuna faida hata moja vyote ni ubatili mtupu, usidanganyike na mambo
ya muda mfupi tu ambayo mwisho wake ni mbaya mnoo.
Unapokuwa mbali
na Mungu na Yeye anakuwa mbali na wewe, unapokuwa karibu na shetani naye
anakuwa karibu na wewe . Mpendwa chagua kuwa karibu na Mungu.
Kusudia kugeuka(Tubu)
kuanzia sasa na umfate Bwana Yesu kuwa
ndiyo mwokozi wa maisha yako( Ufunuo 2:5
imeandikwa;- Basi kumbuka ni wapi
ulipoanguka ukatubu, uyafanye matendo ya
kwanza. Lakini usipofanya hivyo ,naja kwako nami nitakiondoa kinara chako
katika mahali pake usipotubu.
Ubarikiwe
sana mpendwa
@Msufu-January
21, 2021 www.msufu.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni