Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2023
  SOMO # 13: FURAHA ISIYO NA UKOMO Heri ya mwaka mpya Wapendwa! Wapendwa siku zote katika Maisha haya tunayoishi hapa duniani wakati mwingine huwa tunapitia changamoto nyingi sana mpaka zinapelekea kukosa furaha kwa kipindi furani, baada ya kusahau furaha hurudi tena. Lakini siku ya leo Mungu anatuambia katika kitabu cha 1 Wathesalonike 5:16 kwamba;- Furahini siku zote .   Neno hilo ‘Furahini siku zote’ lina maana kubwa sana katika Maisha yetu endapo kama tutalichukulia kwa uzito mkubwa sana. Mungu kusema hivyo sio kwamba hajui kama huwa wakati mwingine tunapata changamoto ambazo zinatuondolea furaha. Lakini Yeye anatamani tuzichukulie hizo changamoto kama ni sehemu ya Maisha kwani huwa zinamwisho kwahiyo zisituondolee furaha ndani ya mioyo yetu.   Mpendwa tambua kwamba Unapokuwa na Yesu kisawasawa ndani yako na ukapata changamoto inatakiwa usiiangalie hiyo changamoto maana itakuondolea furaha bali mwangalie Yesu ,yeye ndio ataiangalia hiyo changamoto na kuin...