Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2023
 SOMO # 18:  SOMO: ITAMBUE MAANA HALISI YA KUMPENDA MUNGU Utangulizi: Watu wengi sana wamekuwa wakisema wanampenda Mungu lakini ukiangalia uhalisia wa maisha wanayoyaishi na wanachokiongea inakuwa ni tofauti kabisa. Mtu anasema anampenda/anamheshimu Mungu lakini ukiingalia moyo wake upo mbali naye kutokana na matendo mabaya anayoyatenda kama ilivyoandikwa katika kitabu cha MATHAYO 15:8-9 kwamba; 8. Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali name, 9. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu. Vile vile imeandikwa katika kitabu cha ISAYA 23:13-15 kwamba; 13. Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa; 14. kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa. 15. Ole wao...