SOMO # 02: MSAMAHA
Mpendwa nakusalimu katika jina la Yesu Kristo. Mpedwa hakuna mtu aliyekamilika kila mtu anamadhaifu katika maisha , kutokana na kuwa tunamadhaifu mengi ,kwahiyo kukoseana/kutofautiana ni lazima kuwepo tu. Kwa minajili hiyo ni lazima sasa tuweze kuachilia msamaha kwa wale wanaotukosea au tuliowakosea kuwaomba msamaha ili Mungu nasi aweze kutusamehe makosa yetu. Maana katika MATHAYO 6:14-15 imeandikwa;- 14 . Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 . Bali msipowasamehe watu makosa yao na Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Mpendwa hayo maneno kutoka Mathayo sio mageni kwako wala neno msamaha sio geni kwako, tambua kuwa neno msamaha linamaana kubwa sana katika maisha yetu ili kuboresha upendo baina yetu sisi na mbele za Mungu. Pia katika MARKO 11:25-26 imeandikwa;- 25 . Ninyi kila msimamapo na kusali sameheni mkiwa na neno juu ya mtu ili na Baba yenu aliye mbinguni awasemehe na ninyi makosa yenu. 26 . Lakini kama nin...