SOMO # 01: ADUI
BWANA YESU ASIFIWE MPENDWA
Mpendwa bila shaka u mzma wa afya kama hali sio nzuri basi Bwana atakuponya tu. Nakukaribisha katika somo hili
Somo linatoka katika kitabu cha ZABURI 143:9 kama ilivyoandikwa;- Ee Bwana uniponye na adui zangu nimekukimbilia wewe unifiche.
Mpendwa tumezungukwa na maadui wengi sana katika Maisha yetu, maadui hao tunaishi nayo na wengine hawaonekani kwa macho yetu.
Je utamjuaje adui yako???
1. Anayekuwazia mabaya ,huyo ni adui yako.
2. Anayekusengenya ,huyo ni adui yako.
3. Anayekuchukia bila sababu,huyo ni adui yako.
4. Anayekugombanisha na watu,huyo ni adui yako.
5. Anayekusema mabaya ,huyo ni adui yako.
6. Anayetaka usiolewe/ usiowe, huyo ni adui yako.
7. Anayetaka uanguke kiimani au huduma yako ife, huyo ni adui yako.
8. Anayetaka ufe siku yoyote, huyo ni adui yako.
9. Anayetaka upate ajali, huyo ni adui yako.
10. Anayetaka biashara yako ife au ufirisike, huyo ni adui yako.
11. Anayetaka ufukuzwe kazi, huyo ni adui yako.
12. Anayetaka ufeli mitihani yako au ufukuzwe shule/chuo ,huyo ni adui yako.
13. Anayetaka ushushwe cheo ofisini, huyo ni adui yako.
14. Anayekudharau muda wote, huyo ni adui yako.
15. Mchawi,Mwizi,Tapeli n.k, hao wote ni adui zako.
Mpendwa kuna aina tatu za maadui ambazo ni;-
1. Maadui wanao onekana.
Hawa ni aina ya adui ambao tunaishi nao katika ulimwengu huu huu tuliopo sisi
Mfano. Wezi, majambazi, matapeli, wabakaji,wasengenyaji, wafitinishaji n.k
2. Maadui wasio onekana.
Hawa ni aina ya maadui ambao huishi katika ulimwengu wa giza yaani hatuwezi kuwaona kwa macho yetu.
Mfano: Majini, Mizimu, Mapepo n.k
3. Maadui ambao nimchanganyiko.
Yaani adui hawa kwa jina lingine ni kinyonga hubadilika badilika kila wanapotaka kufanya uhalifu katika Maisha yetu.
Tunaishi nao lakini shughuli zao chafu huzifanya katika ulimwengu wa giza, na kwa mkitadha huo hatuwezi kuwaona kwa macho yetu wanapotekeleza uhalifu wao.
Mfano wa watu hawa haswa haswa ni Wachawi.
Mpendwa tumezungukwa na maadui kila kona ni Mungu tu ndiye anayeweza kutuepusha na hao maadui wote ambao wapo kinyume na vile tutakavyo sisi katika Maisha yetu, kama katika LUKA 1:74 ilivyoandikwa;- Ya kwamba atujalia sisi tuokoke mikononi mwa adui zetu na kumwabudu pasipo hofu.
Kwahiyo kutokana na huo msitari tunaona ni Mungu ndio anayeweza kutuepusha na hila za adui kwa kumuamini na kumuomba pasipo na mashaka yeyote.
Pia tambua kwamba adui anaweza kuwa Rafiki yako, ndugu yako, mfanyakazi mwenzako, mwanafunzi mwenzako, jirani yako, mfanya biashara mwenzako n.k , hata katika MATHAYO 10:36 imeandikwa;- Na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
Hivyo basi unayecheka naye au kutembea naye , huyohuyo ndio baadaye anakugeuka na kuwa adui yako. Kwahiyo mchague Mungu kwani Yeye hawezi badilika.
Maadui hawakwepeki wapo tu, lakini kinachotupasa kufanya ni kumcha Mungu tu kwa moyo thabiti , baada ya hapo kila adui atakachokua akitaka kukifanya katika Maisha yetu Mungu atatulinda na hakuna adui atakacho fanikiwa kwetu kabisa maana Mungu ndio atakuwa kinga yetu.
Ubarikiwe sana kwa kuusoma ujumbe huu.
Kwa Maswali au Maoni Tuwasiliane kwa no. 0753255132
AMANI YA BWANA WETU YESU KRISTO IWE PAMOJA NAWE.

Zifuatazo ni sifa 15 za aliye adui yako, ukiziona hizo jua tu huyo ni adui wako pasipo hata kuuliza.
1. Anayekuwazia mabaya ,huyo ni adui yako.
2. Anayekusengenya ,huyo ni adui yako.
3. Anayekuchukia bila sababu,huyo ni adui yako.
4. Anayekugombanisha na watu,huyo ni adui yako.
5. Anayekusema mabaya ,huyo ni adui yako.
6. Anayetaka usiolewe/ usiowe, huyo ni adui yako.
7. Anayetaka uanguke kiimani au huduma yako ife, huyo ni adui yako.
8. Anayetaka ufe siku yoyote, huyo ni adui yako.
9. Anayetaka upate ajali, huyo ni adui yako.
10. Anayetaka biashara yako ife au ufirisike, huyo ni adui yako.
11. Anayetaka ufukuzwe kazi, huyo ni adui yako.
12. Anayetaka ufeli mitihani yako au ufukuzwe shule/chuo ,huyo ni adui yako.
13. Anayetaka ushushwe cheo ofisini, huyo ni adui yako.
14. Anayekudharau muda wote, huyo ni adui yako.
15. Mchawi,Mwizi,Tapeli n.k, hao wote ni adui zako.
Aina za Maadui.
Mpendwa kuna aina tatu za maadui ambazo ni;-
1. Maadui wanao onekana.
Hawa ni aina ya adui ambao tunaishi nao katika ulimwengu huu huu tuliopo sisi
Mfano. Wezi, majambazi, matapeli, wabakaji,wasengenyaji, wafitinishaji n.k
2. Maadui wasio onekana.
Hawa ni aina ya maadui ambao huishi katika ulimwengu wa giza yaani hatuwezi kuwaona kwa macho yetu.
Mfano: Majini, Mizimu, Mapepo n.k
3. Maadui ambao nimchanganyiko.
Yaani adui hawa kwa jina lingine ni kinyonga hubadilika badilika kila wanapotaka kufanya uhalifu katika Maisha yetu.
Tunaishi nao lakini shughuli zao chafu huzifanya katika ulimwengu wa giza, na kwa mkitadha huo hatuwezi kuwaona kwa macho yetu wanapotekeleza uhalifu wao.
Mfano wa watu hawa haswa haswa ni Wachawi.
Mpendwa tumezungukwa na maadui kila kona ni Mungu tu ndiye anayeweza kutuepusha na hao maadui wote ambao wapo kinyume na vile tutakavyo sisi katika Maisha yetu, kama katika LUKA 1:74 ilivyoandikwa;- Ya kwamba atujalia sisi tuokoke mikononi mwa adui zetu na kumwabudu pasipo hofu.
Kwahiyo kutokana na huo msitari tunaona ni Mungu ndio anayeweza kutuepusha na hila za adui kwa kumuamini na kumuomba pasipo na mashaka yeyote.
Pia tambua kwamba adui anaweza kuwa Rafiki yako, ndugu yako, mfanyakazi mwenzako, mwanafunzi mwenzako, jirani yako, mfanya biashara mwenzako n.k , hata katika MATHAYO 10:36 imeandikwa;- Na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
Hivyo basi unayecheka naye au kutembea naye , huyohuyo ndio baadaye anakugeuka na kuwa adui yako. Kwahiyo mchague Mungu kwani Yeye hawezi badilika.
Maadui hawakwepeki wapo tu, lakini kinachotupasa kufanya ni kumcha Mungu tu kwa moyo thabiti , baada ya hapo kila adui atakachokua akitaka kukifanya katika Maisha yetu Mungu atatulinda na hakuna adui atakacho fanikiwa kwetu kabisa maana Mungu ndio atakuwa kinga yetu.
Ubarikiwe sana kwa kuusoma ujumbe huu.
Kwa Maswali au Maoni Tuwasiliane kwa no. 0753255132
AMANI YA BWANA WETU YESU KRISTO IWE PAMOJA NAWE.
Ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu Msufu kwa ujumbe mzuri.
JibuFutaNipende kuongezea tu jambo moja la msingi kwamba kama wana wa Baba yetu aliye mbinguni imetupasa tukumbuke kuwapenda adui zetu siku zote na kuwaombea wote wanaotuudhi.
Maoni haya yameondolewa na mwandishi.
FutaUbarikiwe sana mpendwa
JibuFutaUbarikiwe sana mtumishi wa mungu aliye juu Sanaa kwa ujumbe mzuri na unaotia Moyo!!never give up!!Bwana Yesu aliye Munguu peke yupamoja nawe
JibuFuta