SOMO # 02: MSAMAHA
Mpendwa nakusalimu katika jina la Yesu Kristo.
Mpedwa hakuna mtu aliyekamilika kila mtu anamadhaifu katika maisha , kutokana na kuwa tunamadhaifu mengi ,kwahiyo kukoseana/kutofautiana ni lazima kuwepo tu.
Kwa minajili hiyo ni lazima sasa tuweze kuachilia msamaha kwa wale
wanaotukosea au tuliowakosea kuwaomba msamaha ili Mungu nasi aweze
kutusamehe makosa yetu. Maana katika MATHAYO 6:14-15 imeandikwa;- 14.Kwa
maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe
ninyi. 15. Bali msipowasamehe watu makosa yao na Baba yenu hatawasamehe
ninyi makosa yenu.
Mpendwa hayo maneno kutoka Mathayo sio mageni kwako wala neno msamaha sio geni kwako, tambua kuwa neno msamaha linamaana kubwa sana katika maisha yetu ili kuboresha upendo baina yetu sisi na mbele za Mungu. Pia katika MARKO 11:25-26 imeandikwa;- 25.Ninyi kila msimamapo na kusali sameheni mkiwa na neno juu ya mtu ili na Baba yenu aliye mbinguni awasemehe na ninyi makosa yenu. 26. Lakini kama ninyi hamsamehe wala Baba yenu aliye mbinguni hata wasamehe ninyi makosa yenu.
Tumekuwa tukiingia katika maombi ili Mungu aweze kutusamehe dhambi zetu LAKINI ametuambia hataweza kutusamehe makosa /dhambi zetu hali yakwamba sisi tunakuwa hatujawasemehe waliotukosea au hatujaomba msamaha kwa tuliowakosea ili watusamehe.
Mpendwa kukoseana kupo tu ni sehemu ya maisha, tutambue kuwa sehemu yeyote yenye mkusanyiko wa watu kuanzia wawili na kuendelea huwa kutofautiana lazima kuwepo... kwahiyo MSAMAHA siku zote ni endelevu katika maisha yetu kutokana na kuwa tunaishi na jamii yenye watu wa tambia mbali mbali, mitizamo mbalimbali, malezi mbalimbali,elimu mbalimbali, imani mbalimbali n.k. wala hatuishi peke yetu siku zote.
Yamkini tumekuwa tukiingia katika maombi LAKINI maombi hayo yamekuwa hayafanikiwi, yaan hayazai matunda wala hayaleti mabadiliko yeyote katika maisha yetu...kumbe Baba yetu aliye Mbinguni hayajibu maombi hayo kwa sababu tunakuwa hatujaachilia msamaha kwa tuliowakosea au kuwasamehe waliotukosea.
Unaweza ukawa umekosewa na ndugu wa damu, au ndugu wa kawaida, jirani,rafiki,mwanafunzi mwenzako, mfanyakazi mwenzako,mfanya biashara mwenzako n.k .Mpendwa nakuomba uachiliye msamaha hata kama hajakufuata kukuomba msamaha ,wewe mwambie kuwa umemsamehe pasipo kujali ni kosa la aina gani alilokukosea Kwani hata YESU aliwasamehe wayahudi waliomuweka katika mateso yale katika msalaba pasipo kujali amepata maumivu kiasi gani alisema Mungu wasamehe hawajui walitendalo.

AINA YA MSAMAHA
Mpendwa tambua kuwa Mungu anamsamaha wa aina moja tu , lakini sisi wanadamu huwa hatuna msahama wa aina moja kutoka na jinsi ya huruka tuipatayo baada ya kuwa kumetendewa vibaya au tumewatendea watu vibaya, kwahiyo kitokana na hivyo ndio imepelekea kuwa na aina zaidi ya moja ya msamaha utokao kwa wanadamu ( wakristo hata kwa wasio wakristo)
Aina 5 za msamaha ni kama zifuatayo;-
1. MSAMAHA HALISI/ THABITI
Mpendwa huo ni aina ya msahama ambao Mungu ndio huwa anaachilia kwetu baada ya kumuomba msamaha. Katika msamaha huo Mungu anaposamehe huwa hakumbuki tena makosa yetu, katika ISAYA 43:25 imeandikwa;- Mimi, naam ,Mimi ndimi niyafuaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe wala sitazikumbuka dhambi zako.
Kwhyo tunaona kuwa Mungu huwa hakumbuki tena dhambi za wanadamu anaposamehe, pia katika WAEBRANIA 8:12 imeandikwa;- Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikumbuka tena.
Mpendwa ndio maana unaitwa msamaha halisi maana yake kwamba kila anayesamehe hapaswi kuanza kukumbuka tena yale makosa ya nyuma. Kwahiyo katika aina hii ya msamaha wapo hata Wakristo au wasio wakristo huwa wakisamehe hawakumbuki tena ya nyuma na wanaaza moja tena kuwa na maisha ya upendo...Hivyo basi mpendwa tunashauliwa kuwa tuwe na aina ya msamaha wa namna hii maana hata Mungu ndio hutumia aina ya msahama huu, mara tufanyavyo hivyo na Mungu huachiliwa kila jema alitakalo kwetu ililiweze kutendeka katika maisha yetu.
2. MSAMAHA USIO HALISI
Huu ni msahama ambao mtu akisamehe baadaye anaanza tena kuyakumbuka yale aliyosamehe hatimae anaanzisha tena chuku kwa yelu aliyemsamehe kwa maana maumivu yanakuwa yamerudi kutokana na jinsi alivyotendewa.
Mpendwa Hatupaswi kukumbuka makosa ya nyuma ambayo tulishayasamehe kwa sababu huleta maumivu na hasira tena na kusababisha yule uliyemsamehe kuanza kumuona adui kwa kumchukia hali ya kuwa tayari ulishamwambia kuwa ulimsamehe awali.
Hivyo basi mpendwa Mungu haitaji aina ya msamaha wa namna hii maana hauleti matunda yeyote katika maisha yetu ya Kikristo zaidi ya kujenga chuki na uadui kwa waliotukosea japokuwa tunakuwa tayari tulishasema tumesamehe.
3. MSAMAHA WA UONGO
Huu ni msahama ambao hutofautiana kidogo na wa 2 kwa sababu msamaha wa namna hii mtu husema amesamehe mdomoni tu ilikumlizisha yule alimasemehe kumbe ki uhalisia mtu wa namna hiyo anakuwa hajasamehe kabisa kutoka ndani ya moyo wake...huu tunaweza sena ni msamaha wa "danganya toto" kwamba umedanganya kuwa tayari umesamehe lkn moyoni mwako unakuwa unajua kabisa hujasamehe.
Wakristo wengi na wasio wakristo huutumia msamaha wa namna hii pasipo kujua wao...yaani unakuwa umempa mtu matumaini ya kuwa tayari umemsamehe kumbe hakuna chochote ki vitendo...kama ni chuki itaendelea kama kawaida.
Pia msamaha wa namna hii tunaweza uita ni msahama wa kunafiki kwa sababu umesamehe kwa maneno tu lakn chuki bado IPO palepale. Mfano ni kama vile unasema unampenda mtu kutoka mdomoni ilikumlizisha kumbe kiuhalisia humpendi kabisa na nafsi yako inakuwa inajua.
Aina ya msamaha huu unaweza tokea pale mtu anapokuwa amelazimishwa kusamehe na wazazi au marafiki,majirani,ndugu, wanafamiliya n.k ,au mtu anasema amesamehe ili aweze kupata kitu fulan kutoka kwa huyo aliyemwambia amemsamehe akishapata tu hicho kitu basi chuki hurudi palepale.
Hivyo basi mpendwa Mungu haitaji msamaha wa uongo katika Ukristo ,bali anahitaji wote tuwe wakwel katika kusamehe ilituweze kuishi kwa amani katika maisha yetu ya Kikristo na watu wote.
4. MSAMAHA WA MASHARITI.
Huu ni msamaha ambao mtu anayesamehe huweka vigezo na mashariti kwa anayemsamehe, msamaha wa namna hii ndio watu wengi huutumia pia katika jamii yetu tunayoishi.
Mfano: utakutaka mtu anasema nimekusamehe lakini sitakusahau, nimekusamehe lakini staki kianzia sasa unipigie simu yangu na ufute namba kabisa, nimekusamehe lakini sitaki ufike kwangu kuanzia Leo, nimekusame lakini sitafika kwako tena au sitakuomba chochote,nimekusamehe lakini sitaki uje uniombe chochote n.k
Kwahiyo msamaha huu huambatana na hasira ...pia neno "LAKINI" hutumika kwenye msamaha huu.
Mpendwa msamaha wa namna hii sio msamaha ambao Mungu anahitaji tuuachiliye kwa walitukosea kutokana na kuendeleza ugomvi kwa kuweka mashiriti au mikapa kwa msamehewa, ambapo inakuwa haileti Upendo wowote kati ya Msamehe na Msamehewa.
Kwahiyo tunaposamehe tusiweke mashariti yeyote kwan inakuwa hatujasamehe chochote zaidi ya kuwa tumetoa mashariti tu na inakuwa ni chukizo mbele ya Baba yetu Yesu Kristo.
5. MSAMAHA WA KULIPIZA KISASI.
Msamaha wa namna hii huambatana na kulipiza KISASI kwanza kabla ya kusamehe. Kwahiyo mtu ili atake kusamehe ni lazima alipize kisasi ili hasira zimuishe ndio asamehe.
Kwa mfano: Kama mtu kapigwa na yeye anaenda kumpiga huyo mtu kwanza ndio anamsamehe, kama mtu kaiba na yeye anaenda kumuibia kwanza halafu ndio anamsamehe, kama mtu kamkanyaga na yeye anamkanyaga kwanza ndio anamsemehe, kama mtu kamtukana na yeye anamtukana kwanza ndio anamsamehe n.k
Watoto wanaweza kuwa wanacheza gafla mtoto mmoja akampiga mwingine ,mara mzazi wa yule mtoto aliyepigwa akafika ,iliaweze kulizika yule mama utasikia unamwambia yule mtoto haya na wewe mpige ,akisha mpiga yule mama ndio atamsamehe yule mtoto ambaye alimpiga mwanaye.
Kwahiyo msamaha wa namna hii sio mzuri kama wewe umeamua kumsamehe mtu msamehe tu pasipo lipiza kisasi maana katika MITHALI 20:22 imeandikwa;- Usiseme Mimi nitalipa mabaya ,mgojee Bwana naye atakuokoa.
Kwhyo wewe samehe tu, hayo mabaya uliyotendewa Mungu atajua afanye nini zidi ya aliyekutendea.
Mwisho:
Mpendwa Mungu anatupenda wote pasipo kubagua yeyote katika maisha yetu, hivyo basi nasi yatupasa kuwapenda wote na kuachilia msamaha kwa wale ambao walitukosea au watakao tukosea maana tunaishi jamii ya watu wengi kuhitirafiana lazima kuwepo tu.
Pia tambua kabisa Mungu hahitaji msamaha usio halisi, msamaha wa uongo, msamaha wa mashariti na msamaha wa kulipiza kisasi BALI anahitaji msamaha HALISI ilituendelee kudumisha Upendo katika jamii tunayoishi pamoja na kudumisha Upendo kwa Baba yetu Yesu Kristo.
Jichunguze ulishasamehe wangapi, na ulitumia msamaha wa aina gani,baada ya hapo chukua hatua kwa kufuata msamaha uliothabiti ambao utaendeleza kudumisha Upendo kati yako na watu wote pamoja na Yesu Kristo.
UBARIKIWE
Maoni
Chapisha Maoni