Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2019

SOMO #6: MAANA HARISI YA KUMCHA/KUMPENDA MUNGU.

Mpendwa natumaini u mzima wa afya tele na Kama unachangamoto ya ki-afya Mungu ataachilia uponyaji kwako kwa jina la Yesu Kristo aliye hai. Kutokana na kichwa cha somo hapo juu Watu wengi Sana tumekuwa tukisema tunampenda Mungu lakini ukiangalia uharisia wa tunachokiongea na tunachokiishi ni tofauti kabisa . Mungu huwa hapendwi kwa maneno tu pasipo kuyatenda anayotuagiza tuyatende katika maisha yetu. Maana mbili harisi za kumpenda Mungu. 1. Kuchukia uovu MITHALI 8:13a imeandikwa;- Kumcha Bwana ni kuchukia uovu. Mpendwa maana harisi ya kumpenda Mungu ni kuchukia uovu yaani dhambi za hii dunia. i. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kufanya uzinzi? ii. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kunywa pombe? iii. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda rushwa? iv . Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kubaka? v. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda wizi na ujambazi? vi. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda uchawi? vii. Utasemaje un...

SOMO #5: USIKIAJI NA UTENDAJI WA NENO LA MUNGU

Sehemu ya pili. Mpendwa karibu tujifunze muendelezo wa somo lililopita ambalo lilikuwa ni sehemu ya kwanza na leo hii ni sehemu ya pili, vilevile natumaini u mzima wa afya , pole kama unasumbuliwa na changamoto mbalimbali endelea kumuomba Mungu na kumtumainia kwa imani pasipo kukata tamaa Yeye atatenda tu mpendwa. Mpendwa kama tulivyoona somo lililopita kuwa Mungu anatuhitaji tuwe ni watendaji wa Neno ambalo tunalisikia kutoka kwa watumishi mbalimbali makanisani na kwenye mihadhara mbalimbali ya kidini, au Neno tunalolisikiliza kupitia vyombo vya habari, nyimbo za injili n.k vilevile hata Neno tunalolisoma kwenye Biblia Takatifu au kwenye vitabu vya kidini ambavyo vimeandikwa kwa ufasaha na watumishi mbalimbali. Kwahiyo inatupasa tusiishie tu kulisikia Neno au kulikiliza Neno au kulisoma Neno pasipo kulifanyia kazi katika maisha yetu harisia ya hapa duniani tunapoishi wakati wote tukiwa hai. Hii itasaidia kujenga mahusiano mazuri na Mungu na itapelekea Mungu aweze ...