SOMO #6: MAANA HARISI YA KUMCHA/KUMPENDA MUNGU.

Mpendwa natumaini u mzima wa afya tele na Kama unachangamoto ya ki-afya Mungu ataachilia uponyaji kwako kwa jina la Yesu Kristo aliye hai.
Kutokana na kichwa cha somo hapo juu Watu wengi Sana tumekuwa tukisema tunampenda Mungu lakini ukiangalia uharisia wa tunachokiongea na tunachokiishi ni tofauti kabisa .
Mungu huwa hapendwi kwa maneno tu pasipo kuyatenda anayotuagiza tuyatende katika maisha yetu.
Maana mbili harisi za kumpenda Mungu.

1. Kuchukia uovu

MITHALI 8:13a imeandikwa;- Kumcha Bwana ni kuchukia uovu.
Mpendwa maana harisi ya kumpenda Mungu ni kuchukia uovu yaani dhambi za hii dunia.

i. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kufanya uzinzi?
ii. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kunywa pombe?
iii. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda rushwa?
iv . Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kubaka?
v. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda wizi na ujambazi?
vi. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda uchawi?
vii. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kupindisha haki za watu unao wahudumia kwenye hiyo kazi uliyo nayo?
viii. Utasemaje unampenda Mungu wakati muda wote unawaka tamaa mbaya??
ix. Utasemaje unampenda Mungu wakati hata ndugu zako huwapendi? ( Mtu akisema nampenda Mungu na anachukia ndugu yake ni mwongo kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona - 1 Yohana 4: 20)
x. Utasemaje unampenda Mungu wakati hata jirani zako huwapendi kila kukicha wewe ni ugomvi tu?
xi. Utasemaje unampenda Mungu wakati huna muda wa kutetea wajane ,yatima na Mtu yoyote anayeonewa? ( Jifunzeni kutenda mema ,takeni hukumu na haki wasaidieni walioonewa, mpatieni yatima haki yake,mteteeni mjane.- ISAYA 1:17)
xii. Utasemaje unampenda Mungu wakati hata huwa huna muda wa kutubu hizo dhambi zako?
xiii. Utasemaje unampenda Mungu wakati hutaki suruhu Wala kusamehe?
xiv. Utasemaje unampenda Mungu wakati ni mtu wa kupenda kwenda disko na kwenye kumbi zingine za starahe kujistaheresha badala ya kukaa na kumtafakari Yesu Kristo?
Kwahiyo sifa ya mtu anayempenda Mungu ni lazima achukie maovu yote pamoja na kuyakemea wala sio kubakia tu kuongea kwa mdomo wakati moyo wako haupo kwa Mungu , katika MATHAYO 15:8 imeandikwa;- Watu huwa huniheshimu kwa mdomo ila mioyo yao iko mbali nami.
Mpendwa kumpenda Yesu Kristo ni kuachana na maovu yote wala sio kuongea kwa meneno tu.

2. Kuzishika Amri zake.

YOHANA 14:21 imeandikwa:- Yeye aliye na amri zangu na kuzishika yeye ndiye anipendaye naye atapendwa na Baba yangu nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.

Mpendwa amri za Mungu ni Sheria zake na sheria zake ni Neno lake maana ndani ya Neno la Mungu ndio kuna makatazo humo.

Je! Umelishika Neno la Mungu? au unabaki kusema tu unampenda Mungu Hali ya kwamba huna Neno lolote la Mungu ndani ya moyo wako ambalo ndilo litakusaidia kuenenda njia ikupasayo?
Mfano utasemaje unaipenda sheria wakati maneno ya sheria hayapo ndani yako?? Yaani huijui sheria harafu unasema unaipenda sheria!!!!!!

Neno la Mungu ndilo linaelekeza lipi ni jema la kufanya na lipi ni baya la kutolifanya , kumpenda Mungu ni kulishika Neno lake na kulitenda.
Mpendwa ubarikiwe sana na ninakuomba utafakari hili somo na uchukue hatua ya kumpenda Mungu ki-uharisia kwa kuachana na Mambo yote ambayo yanakukosesha vigezo vya Kumpenda Mungu.

AMANI YA BWANA WETU YESU KRISTO IWE PAMOJA NASI.
©Msufu Feb, 2019

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO # 03: MAAJABU YA NAMBA SABA

SOMO # 01: ADUI

SOMO # 07: MAOMBI