SOMO #5: USIKIAJI NA UTENDAJI WA NENO LA MUNGU
Sehemu ya pili.
Mpendwa karibu tujifunze muendelezo wa somo lililopita ambalo lilikuwa ni sehemu ya kwanza na leo hii ni sehemu ya pili, vilevile natumaini u mzima wa afya , pole kama unasumbuliwa na changamoto mbalimbali endelea kumuomba Mungu na kumtumainia kwa imani pasipo kukata tamaa Yeye atatenda tu mpendwa.
Mpendwa kama tulivyoona somo lililopita kuwa Mungu anatuhitaji tuwe ni watendaji wa Neno ambalo tunalisikia kutoka kwa watumishi mbalimbali makanisani na kwenye mihadhara mbalimbali ya kidini, au Neno tunalolisikiliza kupitia vyombo vya habari, nyimbo za injili n.k vilevile hata Neno tunalolisoma kwenye Biblia Takatifu au kwenye vitabu vya kidini ambavyo vimeandikwa kwa ufasaha na watumishi mbalimbali.
Kwahiyo inatupasa tusiishie tu kulisikia Neno au kulikiliza Neno au kulisoma Neno pasipo kulifanyia kazi katika maisha yetu harisia ya hapa duniani tunapoishi wakati wote tukiwa hai. Hii itasaidia kujenga mahusiano mazuri na Mungu na itapelekea Mungu aweze kuyasikia maombi yetu na kututendea baraka mbalimbali ambazo tuna sitahiri kuzipata mbele za Bwana wetu Yesu Kristo aliye hai mile na mile.
Swali # 01:
Je! Mtu yeyote msikilizaji au msomaji wa Neno la Mungu na halifanyii kazi yaani haliweki katika matendo Mungu anamfananishaje mtu huyo?
1. Anafananishwa na mtu Mpumbavu ajengaye nyumba yake juu ya mchanga
MATHAYO 7: 26-27 imeandikwa;-
26. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
27. Mvua ikanyesha mafuriko yakaja ,pepo zikavuma zikaipiga nyumba ile ikaanguka nalo anguko lake likawa kubwa.
Mpendwa ki uharisia mtu mpumbavu ni mtu ambaye anajua kweli kabisa kuhusu jambo Fulani lakini anajifanya hajui kwa kutenda tofauti na ukweli unaotakiwa, hii ni tofauti na mtu Mjinga. Mtu mjinga ni mtu ambaye halielewi jambo Fulani lakini anajifanya analijua jambo hilo, na watu kama hao huwa wabishi sana kwa sababu anaelekezwa ukweli wa jambo lakini yeye anabisha na kubakia na uelewa wake uleule ambao sio sahihi..
Kwahiyo kutokana na misitari hiyo Mungu anamfananisha mtu huyo kuwa ni mpumbavu aliye jenga nyumba yake juu ya mchanga kwa hiyo mvua kubwa ikinyesha na upepo ukipiga basi nyumba ile huanguka, tena Mungu anasema na anguko lake linakuwa ni kubwa sana. Maana yake ni kwamba mtu yoyote anayelisikia Neno la Mungu na akalielewa kabisa lakini halitendei kazi mtu kama huyo kujaribiwa kwake na shetani ni rahisi sana na kuanguka katika dhambi, na akianguka katika dhambi huvutiwa na zile dhambi hatimaye anakuwa anaendelea nazo na si kwamba hafahamu kutenda jambo hilo ni dhambi.
Ni ngumu mtu anayeijua kweli harafu akaiacha kweli na kutenda dhambi ukamhubilia injili kuhusu kuacha dhambi na akacha, inakuwa ni ngumu kuacha dhambi maana tayari mtu huyo analielewa neno lakini anapuuzia tu na ndipo hapo Mungu anapoachilia laana kwa Mtu huyo mpaka kupelekea kutokuacha kutenda dhambi. Lakini ni rahisi mtu asiyeijua kweli kabisa akahubiliwa na akaacha kutenda dhambi maana tayari anakuwa amelisikia Neno ambalo ndiyo kweli ya Bwana Yesu Kristo, japo inakuwa si wote watafanya hivyo.
2. Anafananishwa na mtu anayejiangalia uso wake katika kioo kisha huenda zake mara akasahau jinsi alivyo akarudi tena kujiangalia.
YAKOBO 1:23-24 imeandikwa;-
23. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa Neno tu wala si mtendaji mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
24. Maana hujiangalia kisha huenda zake mara akasahau jinsi alivyo.
Mpendwa mtu kama huyu anakuwa anafananishwa kama mtu msahalifu ,kwahiyo tujitahidi sana kulishika Neno kwa kulitenda tusiwe wasahaulifu kama huyo mtu ambaye hujiangalia kwenye kioo halafu akishaondoka anasahau jinsi ilivyojiona kwenye kioo na anarudi tena kujiangalia. Tuwe na utaratibu wa kuwa na sehemu ya kuandikia ujumbe ili tusiwe tunasahau tulichojifunza maana ki asili sisi wanadamu ni wasahaulifu ndivyo tulivyoumbwa.
Swali # 02:
Je! Mtu yeyote msikilizaji au msomaji wa Neno la Mungu na analifanyia kazi yaani analiweka katika matendo Mungu anamfananishaje mtu huyo?
1. Anafananishwa na Mtu mwenye Akili.
MATHAYO 7:24-25 imeandikwa;-
24. Basi kila asikiaye hayo maneno yangu na kuyafanya atafananishwa na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba .
25. Mvua ikanyesha mafuriko yakaja ,pepo zikavuma zikaipiga nyumba ile isianguke kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba
Mpendwa mtu mwenye akili kikawaida tuna amini kwamba ni mtu ambaye anakumbukumbu ndani ya kichwa chake, yaani ni mtu ambaye ubongo upo sawa na anajitambua akielezwa jambo fulani au kufundishwa hulishika na kulifanya pasipo kusahau au hata akisahau akikumbushwa inakuwa ni rahisi kukumbuka tena kwa mara nyingine.
Ndio maana kuna watu wanaitwa wana mtindio wa ubongo maana yake ni kwamba hawajitambui yaani wanakuwa hawafahamu jema ni lipi na baya ni lipi, watu kama hawa huwa hawafundishiki kwa sababu ya kutokuwa na ufahamu ndani ya ubongo wao.
Kwahiyo kutokana na misitari hiyo Mungu anamfananisha mtu mwenye akili ni Yule ambaye hujenga nyumba yake juu ya mwamba ,mvua ikinyesha kubwa na upepo ukavuma nyumba ile wala haitaweza kudondoka kamwe maana ipo kwenye msingi juu ya mwamba.
Mungu anaposema msingi anamaanisha ni Neno la Mungu na anaposema Mwamba anamaanisha ni Yesu Kristo, hivyo basi mtu unapokuwa na msingi wa Neno la Mungu ambaye Mungu ndiye Mwamba kama ilivyoandikwa katika ISAYA 26:4 kwamba;- Mtumaini Bwana siku zote maana Bwana Yehova ni Mwamba wa milele. ZABURI 89:26 pia imeandikwa:- Yeye ataniita ,Wewe Baba yangu ,Mungu wangu na Mwamba wa wokovu wangu.
Ukilishika Neno hilo kamwe hautaweza kudondoshwa na shetani au na dhambi yoyote maana wewe tayari unaijua kweli na kweli hiyo unaiweka katika matendo, hata jaribu lije la aina gani halitaweza kukutoa kwenye uwepo wa Mungu maana Neno umelishika na hulifanyia kazi na ndipo Mungu hatakuacha uteteleke na jambo lolote baya ambalo lipo mbele yako.
2. Mtu ambaye hubarikiwa na Mungu.
YAKOBO 1:25 imeandikwa;- Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru na kukaa humo asiwe msikiaji msahaulifu bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
UFUNUO 1:3 imeandikwa;- Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyashika yaliyoandikwa humo kwa maana wakati u karibu.
Mpendwa Biblia inaposema Heri(Blessed) maana yake ni ‘’baraka za Bwana’’, mfano ‘’Heri asomaye’’ maana yake ni ‘’Atabarikiwa asomaye’’ kwahiyo mtu yeyote atendaye Neno la Bwana Yesu Kristo ni lazima Mungu ataachiliya baraka zake katika maisha yake, ndio maana Biblia inasema Mungu hana upendelo wale wote wamchao Yeye hawaachi, maana yake ni kwamba Mungu humpatia baraka zake mtu yeyoye anayesikiliza Neno na kulitenda katika maisha yake.
Mtu ambaye imani yake inakwenda na matendo ni lazima maisha yake yawe ya kumpendeza Mungu na Mungu akishapendezwa na mtu ni lazima ataachiliya baraka zake.
Hivyo basi mpendwa tuombe neema ya Mungu iwe ndani yetu ili tuweze kuliishi Neno la Mungu na hatimaye hatutakuwa wapumbavu mbele za Bwana bali tutakuwa ni watu wenye akili na Baraka tele katika maisha yetu.
Ubarikiwe sana kwa kuusoma ujumbe huu mpendwa naamini utakuwa umejifunza au kujikumbusha kitu.
AMANI YA BWANA WETU YESU KRISTO IWE PAMOJA NASI.
© Msufu Feb, 2019.

Maoni
Chapisha Maoni