SOMO #9: MAMBO MUHIMU YA KUYAFANYA KABLA YA KUINGIA MWAKA MPYA 2021. Mpendwa karibu ujifunze somo hili. 1. Mshukuru Mungu kwa yote aliyokutendea na ambayo hajayatenda huu mwaka 2020 1 Wathesalonike 5:18 imeandikwa;- Shukuruni kwa kila jambo ; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Yesu Kristo. 1 Mambo ya Nyakati 16:34 imeandikwa;- Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema kwa maana fadhili zake ni za milele Zaburi 75:1 imeandikwa;- Ee Mungu twakushukuru ,twakushukuru kwa kuwa jina lako li karibu ,watu huyasimuliya matendo yako ya ajabu. Mpendwa, kwahiyo upate au usipate yote hayo ni mapenzi ya Mungu ,hivyo basi Mshukuru kwa vyote. Baadhi ya Mambo ya kushukuru mbele za Mungu ni kama yafuatayo;- i. Kuna mambo Mungu amefanikisha kukutendea ambayo yalikuwa yapo ndani ya malengo yako ya 2020 ii. ...
Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia 2020
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine

SOMO # 8: USILAUMU SONGA MBELE MWAKA 2021 Mpendwa kwanza na kusalimu kwa Jina la Yesu Kristo. Kwanza ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwa kutupa neema ya kuanza mwaka huu 2020 tukiwa wazima toka umeanza mwezi wa kwanza na sasa tupo mwezi wa 12 mwishoni kabisa , haijalishi uliweka MALENGO mengi kiasi gani mwaka huu, na mengine yametimia au hayajatimia mpaka muda huu unapoelekea mwisho wa mwaka au hukuweka Malengo kabisa,Mpendwa usilaumu wala usikate tamaa maana katika kitabu cha MHUBIRI 3:1 imeandikwa kwamba;- Kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya Mbingu . Hivyo basi unapoona malengo yako hayajatimia jua kwamba wakati na majira yake utafika tu na malengo mpaka yatatima katika jina la Yesu Kristo. Mpendwa unaweza ukatafakari, kwa huu mwaka 2020 umefanya jambo gani la maana na unaweza usipate majibu, lakini nakutia moyo kwamba usijilaumu kwa kupoteza muda mpaka mwaka unaenda kuisha bado kuna vitu hujavifanya, lakini tamb...