SOMO
# 8: USILAUMU SONGA MBELE MWAKA 2021
Mpendwa kwanza na kusalimu kwa Jina la Yesu Kristo.
Kwanza ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwa kutupa neema ya kuanza mwaka huu 2020
tukiwa wazima toka umeanza mwezi wa kwanza na sasa tupo mwezi wa 12 mwishoni
kabisa , haijalishi uliweka MALENGO mengi kiasi gani mwaka huu, na mengine
yametimia au hayajatimia mpaka muda huu unapoelekea mwisho wa mwaka au hukuweka
Malengo kabisa,Mpendwa usilaumu wala usikate tamaa maana katika kitabu cha MHUBIRI 3:1 imeandikwa kwamba;- Kwa kila jambo kuna majira yake na wakati
kwa kila kusudi chini ya Mbingu. Hivyo basi unapoona malengo yako
hayajatimia jua kwamba wakati na majira yake utafika tu na malengo mpaka
yatatima katika jina la Yesu Kristo.
Mpendwa unaweza ukatafakari, kwa huu mwaka 2020
umefanya jambo gani la maana na unaweza usipate majibu, lakini nakutia moyo
kwamba usijilaumu kwa kupoteza muda mpaka mwaka unaenda kuisha bado kuna vitu
hujavifanya, lakini tambua kwamba mwaka 2021 ndiyo huo unakuja hivyo basi weka
MALENGO yako na uyaombee, Mungu atayatakabali.
Inawezekana uliweka malengo yako vizuri kabisa mwaka
huu 2020 lakini ikatokea ukapata changamoto ya kiafya labda mpaka sasa unaumwa ,
au yakifedha au migogoro ikatokea au ukakosa shauku kabisa ya kutekeleza
malengo yako, mpendwa nataka kukwambia kwamba endelea kumtumainia Mungu wala
usikate tama kwa kulaumu( ZABURI 125:1
imeandikwa;- Wamtumainio Bwana ni kama
mlima Sayuni ambao hautatikisika, wakaa milele) ninakuombea mwaka 2021
Mungu akakushangaze katika jina la Yesu Kristo, maana mawazo anayo kuwazia wewe
ni mawazo mema kabisa wala sio mabaya kama ilivyoandikwa katika kitabu cha YEREMIA 29:11 kwamba;- Maana nayajua mawazo ninayokuwawazia ninyi,
asema Bwana ni mawazo ya amani wala si ya mabaya ,kuwapa ninyi tumaini siku
zenu za mwisho.
Vilevile unaweza ukawa uliweka malengo yako lakini kuna watu(marafiki,majirani,ndugu
n.k) walikuja kukukatisha tamaa au
mazingira uliyopo yalikukatisha tamaa na mpaka sasa hakuna ulichofanya au
umefanya kidogo, mpendwa nataka kukwambia kwamba mwaka 2021 Mungu anaenda
kukushangaza katika jina la Yesu Kristo. Wewe endelea tu kumtumaini maana Yeye macho
yake yapo kila mahali anakuona mpendwa wala usijali kwa kuhangaika kwako yaani umekata
tamaa au umebaki kujilaumu tu tambua kuwa neema ya Mungu bado ipo katika maisha yako( MITHALI 15:3 Macho ya Bwana yapo kila mahali yakimchunguza mbaya na mwema),
lakni pia Biblia inasema katika ZABURI
23:6 kwamba;- Hakika wema na fadhili
zitanifuata siku zote za maisha yangu ,nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
Mpendwa nami ninakuombea katika jina la Yesu Kristo wema na fadhili za Bwana
vikufuate mwaka 2021 popote ulipo wewe unayesoma ujumbe huu kama jinsi Neno
lake Bwana linavyosema katika Zaburi 23:6 Amen.
Licha ya hivyo inawezekana malengo uliyoyaweka mwaka huu 2020 hukuanza
kwa kuyatanguliza mbele za Mungu yaani hukumkabidhi Mungu, ila ukaanza
kuwaambia kwanza watu wako wa karibu hatimaye ndiyo ikafikia hatua ya Malengo
yako kuvurugika kabisa na kukatishwa tamaa kukawa kwingi, yaani ikawa ni
tofauti na ulivyotegemea wewe.
Nataka kukwambia kwamba MALENGO yako yote ya mwaka
2021 cha kwanza inatakiwa umkabidhi Bwana Yesu ili aweze kuyabariki , kuyalinda
na kukutia Ujasiri na Nguvu unapokwenda kuyatekeleza katika huo mwaka mpya (ZABURI 37:5 imeandikwa;- Umkabishi
Bwana njia yako, pia umtumaini naye atafanya.)
Mpendwa kama tulivyouona huo mstari kutoka Zaburi
37:5 kwamba Mungu anaposema umkabidhi NJIA YAKO, maana yake kwamba NJIA ndio
mambo( MALENGO) yako yote unayotaka kuyafanya cha kwanza inatakiwa uyapeleke mbele
za Mungu ili yakapate kibali ( ZABURI
19:14 imeandikwa;- Maneno ya kinywa
changu na mawazo ya moyo wangu yapate kibali mbele zako, Ee Bwana mwamba wangu
na mwokozi wangu. ) Usianze kwanza kuwaambia watu malengo yako kabla
hujayakabidhi mbele za Mungu, kama hutaanza kumkabidhi Mungu hapo ndipo shetani
atakapopata nafasi ya kuyakwamisha malengo yako maana hukuanza kwanza kwa
kumkabidhi Mungu.
Mpendwa nimalizie kwa kusema hivi, kuweka MALENGO(
yaani ya muda mrefu na mfupi) katika
maisha yako ni jambo la muhimu sana maana hata Mungu alipokuwa anaumba dunia na
vitu vyote vilivyomo ndani yake aliweka malengo kwanza kabla ya Kuumba maana
hakukurupuka tu , ndiyo maana ukisoma katika kitabu cha MWANZO 1: 1-31 na 2:1-2 utaona
kwamba Mungu alitumia siku 7(wiki moja) kutimiza MALENGO yake aliyokuwa ameyapanga na kweli
yakatimia ,ukisoma kwa makini mistari hiyo kutoka kitabu cha Mwanzo utaelewa ninachokizungumzia.
MHIMU:
Kabla ya kuweka MALENGO yako ya mwaka
2021 zingatia haya mambo sita(6);
Ubarikiwe sana mpendwa.
@Msufu- Desemba 29, 2020, www.msufu.blogspot.com,
0753255132
Maoni
Chapisha Maoni