Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2018

SOMO # 03: MAAJABU YA NAMBA SABA

 MAAJABU YA NAMBA SABA (7) Mungu ni wa ajabu Sana hakika hakuna mwanadamu awezaye kumchunguza maaana Yeye ndiye mwenye siri kubwa wa hii namba 7 katika ulimwengu wa ki-Roho. Mpendwa tunapoenda kuumalizia huu mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019 naomba tuone haya maajabu makubwa ya namba 7 ambayo Mungu ndio anaijua Siri yake. Na haya maajabu ya namba Saba ninayoenda kuyaandika si kwamba ni yote ila ni kwa uwezo wa kufikiri kwangu na kusoma Biblia vile vile pamoja na Roho Mtakatifu kunipa mzigo wa kuandika somo hili maana nimeanza kuliandaa kwa muda mrefu kidogo. Mpendwa nakujulisha kuwa hili somo ni refu hivyo basi Mungu akusaidie usome kwa umakini pasipo kuishia njiani ili uweze kumaliza. _Mambo hayo ni Kama yafuatayo;-_ 1. Mungu ana Roho 7. UFUNUO 4:5 imeandikwa;- Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti ya ngurumo na taa Saba za Moto zikiwaka  mbele ya kile kiti cha enzi ndizo Roho Saba za Mungu. 2. Kitabu kilicho Mbinguni kina Mihuri 7. UF...

SOMO # 02: MSAMAHA

Mpendwa nakusalimu katika jina la Yesu Kristo. Mpedwa hakuna mtu aliyekamilika kila mtu anamadhaifu katika maisha , kutokana na kuwa tunamadhaifu mengi ,kwahiyo kukoseana/kutofautiana ni lazima kuwepo tu. Kwa minajili hiyo ni lazima sasa tuweze kuachilia msamaha kwa wale wanaotukosea au tuliowakosea kuwaomba msamaha ili Mungu nasi aweze kutusamehe makosa yetu. Maana katika MATHAYO 6:14-15 imeandikwa;- 14 . Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 . Bali msipowasamehe watu makosa yao na Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Mpendwa hayo maneno kutoka Mathayo sio mageni kwako wala neno msamaha sio geni kwako, tambua kuwa neno msamaha linamaana kubwa sana katika maisha yetu ili kuboresha upendo baina yetu sisi na mbele za Mungu. Pia katika MARKO 11:25-26 imeandikwa;- 25 . Ninyi kila msimamapo na kusali sameheni mkiwa na neno juu ya mtu ili na Baba yenu aliye mbinguni awasemehe na ninyi makosa yenu. 26 . Lakini kama nin...

SOMO # 01: ADUI

 BWANA YESU ASIFIWE MPENDWA Mpendwa bila shaka u mzma wa afya kama hali sio nzuri basi Bwana atakuponya tu. Nakukaribisha katika somo hili Somo linatoka katika kitabu cha ZABURI 143:9 kama ilivyoandikwa;- Ee Bwana uniponye na adui zangu nimekukimbilia wewe unifiche. Mpendwa tumezungukwa na maadui wengi sana katika Maisha yetu, maadui hao tunaishi nayo na wengine hawaonekani kwa macho yetu. Je utamjuaje adui yako??? Zifuatazo ni sifa 15 za aliye adui yako, ukiziona hizo jua tu huyo ni adui wako pasipo hata kuuliza. 1. Anayekuwazia mabaya ,huyo ni adui yako. 2. Anayekusengenya ,huyo ni adui yako. 3. Anayekuchukia bila sababu,huyo ni adui yako. 4. Anayekugombanisha na watu,huyo ni adui yako. 5. Anayekusema mabaya ,huyo ni adui yako. 6. Anayetaka usiolewe/ usiowe, huyo ni adui yako. 7. Anayetaka uanguke kiimani au huduma yako ife, huyo ni adui yako. 8. Anayetaka ufe siku yoyote, huyo ni adui yako. 9. Anayetaka upate ajali, huyo ni adui yako. 10. Anayetaka biashar...