Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2019

SOMO # 07: MAOMBI

MAOMBI Utangulizi: Maombi ni mawasiliano kati ya Muombaji na Mungu , Maombi kwa sisi wacha Mungu hayaepukiki maana tukikaa kimya na kusema unampenda Mungu bila Maombi na kusoma Neno ni rahisi Sana kurudi nyuma kiimani maana adui atatushambulia kirahisi mnooo. Na majaribu yatatushambulia mengi mnooo katika maisha yetu na tutashindwa kuyaepuka kwa sababu hatudumu katika maombi. Baadhi ya watu wengi wamekuwa na mzigo yaani shauku ya maombi pale wanapopata shida Mfano mtu anamuomba Mungu ampe kazi yaani apate ajira, aolewe yaani apate mume, aowe yaani apate mke, apate biashara ya kufanya,apate gari,apate fedha,apate safari labda ya kwenda nje ya nchi au anaumwa ugojwa fulani n.k ndio utamwona yapo bize na Mungu na kanisani haachi kuhudhuria kila Jumapili na hata kwenye zile ibada za katikati ya wiki hakosi Lakini akisha kipata kile anachokihitaji kutoka kwa Mungu kupitia yale Maombi aliyokuwa akiyaomba kila siku, utamwona Maombi amepunguza kabisaaa na hat...

SOMO #6: MAANA HARISI YA KUMCHA/KUMPENDA MUNGU.

Mpendwa natumaini u mzima wa afya tele na Kama unachangamoto ya ki-afya Mungu ataachilia uponyaji kwako kwa jina la Yesu Kristo aliye hai. Kutokana na kichwa cha somo hapo juu Watu wengi Sana tumekuwa tukisema tunampenda Mungu lakini ukiangalia uharisia wa tunachokiongea na tunachokiishi ni tofauti kabisa . Mungu huwa hapendwi kwa maneno tu pasipo kuyatenda anayotuagiza tuyatende katika maisha yetu. Maana mbili harisi za kumpenda Mungu. 1. Kuchukia uovu MITHALI 8:13a imeandikwa;- Kumcha Bwana ni kuchukia uovu. Mpendwa maana harisi ya kumpenda Mungu ni kuchukia uovu yaani dhambi za hii dunia. i. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kufanya uzinzi? ii. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kunywa pombe? iii. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda rushwa? iv . Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda kubaka? v. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda wizi na ujambazi? vi. Utasemaje unampenda Mungu wakati unapenda uchawi? vii. Utasemaje un...

SOMO #5: USIKIAJI NA UTENDAJI WA NENO LA MUNGU

Sehemu ya pili. Mpendwa karibu tujifunze muendelezo wa somo lililopita ambalo lilikuwa ni sehemu ya kwanza na leo hii ni sehemu ya pili, vilevile natumaini u mzima wa afya , pole kama unasumbuliwa na changamoto mbalimbali endelea kumuomba Mungu na kumtumainia kwa imani pasipo kukata tamaa Yeye atatenda tu mpendwa. Mpendwa kama tulivyoona somo lililopita kuwa Mungu anatuhitaji tuwe ni watendaji wa Neno ambalo tunalisikia kutoka kwa watumishi mbalimbali makanisani na kwenye mihadhara mbalimbali ya kidini, au Neno tunalolisikiliza kupitia vyombo vya habari, nyimbo za injili n.k vilevile hata Neno tunalolisoma kwenye Biblia Takatifu au kwenye vitabu vya kidini ambavyo vimeandikwa kwa ufasaha na watumishi mbalimbali. Kwahiyo inatupasa tusiishie tu kulisikia Neno au kulikiliza Neno au kulisoma Neno pasipo kulifanyia kazi katika maisha yetu harisia ya hapa duniani tunapoishi wakati wote tukiwa hai. Hii itasaidia kujenga mahusiano mazuri na Mungu na itapelekea Mungu aweze ...

SOMO # 04: TUWE WASIKILIZAJI NA WATE NDAJI WA NENO LA MUNGU

  TUWE WASIKILIZAJI NA WATE NDAJI WA NENO LA MUNGU Hii ni sehemu ya kwanza katika somo hili. Mpendwa heri ya Mwaka mpya, karibu tujifunze hili somo, Bwana akutanguliye na kukupa uaminifu katika kulisoma na kulichukulia hatua kwenye huu mwaka ili mambo makubwa kabisa kwa imani Mungu aweze kuyatenda katika maisha yako. Mpendwa nakuomba huu mwaka na kuendelea tuachane na ile Tabia ya kulisikiliza Neno la Mungu tu pasipo kulifanyia kazi, Maana tutakuwa hatuna utofauti na wale ambao hawamwamini Mungu na ambao hawaendagi hata kanisani. YAKOBO 1:22 imeandikwa;- Lakini iweni watendaji wa Neno Wala si wasikilizaji tu bali mkijidanganya nafsi zenu. Mpendwa katika maisha yetu mpaka hapa tulipo najua tulishalisikiliza Neno la Mungu katika sehemu na njia mbalimbali Sana LAKINI Je! Hilo Neno huwa tunalifanyia kazi katika maisha yetu?! Je! Neno huwa linasikilizwa wapi? 1. Huwa tunalisikia Neno la Mungu kupitia Waimbaji mbalimbali makanisani kwetu Kila tukienda kusali kuna kwaya h...