SOMO # 04: TUWE WASIKILIZAJI NA WATE NDAJI WA NENO LA MUNGU

  TUWE WASIKILIZAJI NA WATE NDAJI WA NENO LA MUNGU
Hii ni sehemu ya kwanza katika somo hili.
Mpendwa heri ya Mwaka mpya, karibu tujifunze hili somo, Bwana akutanguliye na kukupa uaminifu katika kulisoma na kulichukulia hatua kwenye huu mwaka ili mambo makubwa kabisa kwa imani Mungu aweze kuyatenda katika maisha yako.
Mpendwa nakuomba huu mwaka na kuendelea tuachane na ile Tabia ya kulisikiliza Neno la Mungu tu pasipo kulifanyia kazi, Maana tutakuwa hatuna utofauti na wale ambao hawamwamini Mungu na ambao hawaendagi hata kanisani.
YAKOBO 1:22 imeandikwa;- Lakini iweni watendaji wa Neno Wala si wasikilizaji tu bali mkijidanganya nafsi zenu.
Mpendwa katika maisha yetu mpaka hapa tulipo najua tulishalisikiliza Neno la Mungu katika sehemu na njia mbalimbali Sana LAKINI Je! Hilo Neno huwa tunalifanyia kazi katika maisha yetu?!
Je! Neno huwa linasikilizwa wapi?
1. Huwa tunalisikia Neno la Mungu kupitia Waimbaji mbalimbali makanisani kwetu Kila tukienda kusali kuna kwaya huwa zinaimba.
2. Huwa tunalisikia Neno la Mungu kwa wahubiri mbalimbali kwenye makanisa yetu.
3. Huwa tunalisikia Neno kwa kushuhudiwa na watu mbalimbali sehemu tulipo labda kwenye biashara zetu au kwenye kazi zetu au tuwapokuwa safarini au tuwapo sokoni.
4. Huwa tunalisikia Neno la Mungu na kulisoma katika Biblia tuwapo kanisani na tuwapo nyumbani.
5. Huwa tunalisikia Neno la Mungu kwenye vyombo vya habari yaani T.V na Radio hata kwenye magazeti.
6. Huwa tunalisikia Neno la Mungu kwenye Seminar na mikutano mbalimbali ya wahubiri
7. Huwa tunalisikia Neno kupitia CD za watu waliorekodi tuwapo majumbani kwetu au kwenye biashara zetu au safarini au kazini kwetu. N.k
Tutafakari Maswali.
1. Je! Huwa tunalifanyia kazi hilo Neno tulisikiapo???
2. Au huwa tunaishia tu kulisikia Neno kwa kufarahia mtu anapocheza au kufarahia tu mdundo wa mziki kama ni kwaya??
3. Au huwa tunaishia tu kulisikiliza Neno na kumwangaliya tu yule anayelitoa na kuanza kumtathimini kuliko kulitathimini Neno la Mungu??
4. Au huwa tunamdharau yule anayehubiri lile Neno labda tunamfahamu maisha yake ya nyuma yalivyokuwa mabaya pasipo kujua tayari Mungu alishambadilisha???
5. Au labda tunajiona tayari tunafedha na maisha mazuri kwahiyo hatulihitaji Neno la Mungu litende baraka katika maisha yetu??
6. Au tunaona kwamba hakuna faida yeyote ya kulitendea kazi Neno la Mungu maana tunajiona tupo salama Kila siku pasipo kujua ni Mungu ndiye anayetupa uhai huu tulionao Kila siku??
7. Au tunatamani kulitendea Kazi Neno la Mungu kwa kukifuata Kila tunachohubiriwa lakini kunamadhaifu ya mwili ambayo yanatuzuia tusiweze kulifanyia kazi Neno???
8. Au kuna majaribu ambayo yanatuzuia kulifanyia kazi Neno la Mungu mara tulisikilizapo??
9. Au tuna vikundi vibaya vya marafiki ambao wanatuzuia na kutushawishi kuishi maisha mabaya na hatimaye kuishia tu kulisikiliza Neno na kutolitendea kazi??
10. Au mazingira tunayoishi ndio yanatuzuia tusilifanyie kazi Neno la Mungu Mara tunapolisikia??
N.k
Mpendwa sikiliza nikwambiye Mungu yupo na Kama yupo basi inatupasa tuishi maisha sawasawa na Neno lake linavyotaka ,ndio tutamuona Yeye akitenda mambo makubwa katika maisha yetu pamoja ja na kwenye familiya zetu .
Pia Inatupasa tuwapo makanisani au mahali popote tuendapo tuwe na notebook au daftari la kuwa tunaandikia Neno la Mungu Mara tulisikiapo au kulisomapo ili kuweka kumbukumbu vizuri kwa ajili ya kulifanyia kazi kwa vitendo.
Maana katika YAKOBO 2:26 imeandikwa;- Maana kama vile mwili pasipo Roho umekufa, vivyo hivyo na Imani pasipo matendo imekufa.
Imani maana yake ni kwamba kile unacho kiamini kupitia Neno la Mungu inakupasa ukitende na sio kuishia tu kusema Mimi na Mwamini Mungu kwa maneno bila utendaji...je! unamwamini Mungu au unampenda Mungu kwa lipi na kivipi?? Maana katika YOHANA 14: 15 & 23
15. Mkinipenda mtazishika amri zangu.
23. Yesu kajibu akamwambia mtu akinipenda atalishika Neno langu na Baba yangu atampenda ,nasi tutakuja kwake na kufanya makao kwake.
Kwahiyo Mpendwa Kumwamini na Kumpenda Mungu ni kulishika Neno lake, maana yake ni kulifanyia kazi pasipo kuishia tu kulikiliza na kusahau au kulipuuzia.
Mpendwa somo lijalo tunaona mtu anayelisikiliza Neno na Halitendei kazi au analitendea kazi je! anafanishwaje na Mungu na nini madhara ya kulisikiliza Neno na kutolifanyia kazi??
Ubarikiwe Sana kwa kuusoma ujumbe huu ,Mungu atupe neema ya kulisikiliza na kulitendea Kazi Neno lake hapo ndipo Imani itakuwa imeendana na matendo.
Sehemu ya Pili itaendelea..............
AMANI YA BWANA WETU YESU KRISTO IWE PAMOJA NASI.
©Msufu January, 2019

Maoni

  1. Mungu wa mbinguni akubariki sana. Hakika somo hili limekuwa msaada mkubwa sana kwangu.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO # 03: MAAJABU YA NAMBA SABA

SOMO # 01: ADUI

SOMO # 07: MAOMBI