SOMO # 12   TUNAPOELEKEA KUUMALIZA MWAKA HUU 2022 KWA HIZI SIKU CHACHE ZILIZOBAKI NAOMBA UJITAFAKARI KWA UAMINIFU KUPITIA HAYA MAMBO NILIYOYAANDIKA.

1. Hebu fikiria umesafiri mara ngapi huu mwaka au toka umeanza kusafiri na miaka iliyopita Mungu amekuepusha na ajali ngapi hata zingine bila ya wewe kujua?Na mpaka sasa upo mzima hata kama ulishawahi kupata ajali. Je! Unajua Mungu anamakusudi gani na wewe katika maisha yako mpaka sasa upo mzima?. Je? Unafikiri amekuepusha na haya kwa ajili ya matendo yako ni mazuri sana au kuna kitu ulimpa ili akulinde?. TAMBUA KWAMBA HIYO NI NEEMA NA REHEMA ZA MUNGU KWAKO, USIJISIFU NI MUNGU ANAKUWAZIA MAWAZO YALIYO MEMA SIKU ZOTE WALA SIO MABAYA (Yeremi 29:11- Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho).
2. Hebu fikiria ulitegewa mitego mara ngapi (kwenye chakula, maji, njiani/barabarani,ofisini,biashara n.k) na adui hata bila ya wewe kujua na Mungu akakunusuru na hiyo mitengo?. Je unafikiri hayo yote Mungu aliyokuepusha nayo unafikiri ni kwa akili zako au ujanja wako au matendo yako ni mazuri sana kuwazidi wengine?. TAMBUA KWAMBA HIYO NI NEEMA NA REHEMA ZA MUNGU KWAKO, USIJISIFU MAANA MUNGU AMESEMA ATAWAPIGA ADUI ZAKO MBELE YAKO NA ATAWASAMBALATISHA NA WATAKIMBIA KWA NJIA SABA (Kumbukumbu laTorati 28:7- Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba).
3. Hebu fikiria toka mwaka huu 2022 ulipoanza mpaka hizi siku chache zilizobaki ni mara ngapi uliugua/uliumwa au hujaugua kabisa? Lakini mpaka leo hii Mungu alikupigania na anaendelea kukupigania ,je! Unafikiri ni kwa ajili ya matendo yako ni mazuri sana au ujanja wako wa kuzingatia kanuni za afya?. MPENDWA HIYO NI NEEMA NA REHEMA ZA MUNGU KWAKO, USIJISIFU ILA MUNGU AMESEMA ATAKUONDOLEA MAGONJWA YOTE (Kumbukumbu laTorati 7:15- Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao).
4. Hebu fikiria kwa wewe uliyepo ofisini wamekukalia vikao vingapi ili ufukuzwe kazi au ushushwe cheo au uhamishwe au uangamizwe kabisa bila hata ya wewe kujua lakini Mungu akakupigania?je! unafikiri ni kwa ujanja wako? Hapana, TAMBUA KWAMBA HIYO NI NEEMA NA REHEMA ZA MUNGU KWAKO, USIJISIFU MAANA MUNGU AMESEMA KILA SILAHA ITAKAYOINUKA KWAKO HAITAFANIKIWA KABISA ( Isaya 54:17- Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana).
5. Hebu fikiria wewe unayefanya biashara toka mwaka umeanza biashara yako inaendelea vizuri hata kama ililegalega ila mpaka sasa ipo inaendelea vizuri japokuwa maadui walikukusudua mabaya katika biashara yako lakini Mungu akakupigania hata bila ya wewe kujua,je unafikiri ni kwa ujanja wako ? au bidii zako?.MPENDWA USIJISIFU HIYO NI KWA NEEMA YA MUNGU TU WALA SI VINGINEVYO, MUNGU ANGEWEZA KUAMUA LOLOTE KUSINGESHINDIKANA KITU CHOCHOTE (Mwanzo 18:14a- Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana?).
6. Hebu fikiria wewe unayesoma shule ya msingi au sekondari au chuo ni mambo mangapi Mungu amekuepusha nayo huko kwenye masomo yako? Je! Unafikiri hao wanafunzi wenzako wote wanakutakia mema?. MPENDWA USIJISIFU HIYO NI NEEMA YA MUNGU TU KWAKO IMEKUSHUKUIA WALA SIO KWA UJANJA WAKO MAANA MUNGU AMESEMA ATAKUFANYA KUWA KICHWA WALA SIO MKIA (Kumbukumbu laTorati 28:13- Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya).
7. Hebu fikiria wewe ni dereva wa chombo chochote cha moto, Mungu amekuipusha na ajari ngapi hata zingine bila ya wewe kujua? Je! Unafikiri ni kwa sababu unajua kuendesha sana kuliko wengine? Au unafikiri kwa sababu ya uimara wa chombo chako cha moto?. MPENDWA NI NEEMA YA MUNGU TU NDIO IMEKUBEBA MAANA AMESEMA YEYE ATATULINDA NA MABAYA YOTE ( Zaburi 121:7-8 imeandikwa;- 7.Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. 8. Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele).
8. Hebu fikiria wewe ni mtumishi wa Mungu kama vile Mchungaji au Mwinjilisti au Mwimbaji n.k, je! Mungu amekupigania na kakuepusha na vita vingapi vya adui katika utumishi wako? Au ni wangapi mpaka sasa walishaacha kumtumikia Mungu kwa sababu mbalimbali zilizowakumba? TAMBUA KWAMBA HIYO NI NEEMA TU YA MUNGU IPO UPANDE WAKO YA KUENDELEA KUMTUMIKIA YEYE NA KUKUEPUSHA NA MABAYA MAANA AMESEMA YEYE NI UKUTA WA MOTO ATAUZUNGUSHA KWAKO ILI AKULINDE( Zakaria 2:5- Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake).
MPENDWA KWA TAFAKARI HIZO, SASA NINI CHA KUFANYA?
Yafuatayo ni Mambo ambayo inatakiwa uyafanye ili Mungu aendelee kuachilia neema na rehema kwako mwaka 2023.
1. Achana na matendo yote mabaya ambayo umekuwa ukiyatenda, na kama hujaokoka ni wakati mzuri wa wewe kumkabidhi Bwana Yesu maisha yako, sio kwamba Mungu alikuwa haoni unachokifanya hapana ila ilikuwa ni neema Yake tu ndio ilikuwa inakubeba, maana Mungu anasema Jicho lake lipo kila mahali likimchunguza mbaya na mwema ( Mithali 15:3- Macho ya Bwana yako kila mahali; yakimchunguza mbaya na mwema). Mpendwa usiifiche hiyo dhambi yako maana neno la Bwana linasema afichaye dhambi zake hatafanikiwa (Mithali 28:13 - Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema).
2. Tubu dhambi zako zote ili uingie mwaka 2023 moyo wako ukiwa ni msafi mbele za Bwana, maana Biblia inasema wenye moyo safi ndio watamwona Mungu ( Mathayo 5:8 - Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu). Mpendwa usiogope kutubu maana Mungu anasema uwe na bidii ya kutubu ( Ufunuo 3:19- Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu). Ni wewe ndio unayajua maisha yako unayoyaishi wala si mtu mwingine zaidi ya Mungu, kwa sababu Yeye amesema anayajua matendo yetu (Ufunuo 3:15-16 imeandikwa;- 15. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 . Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa change).
3. Mshukuru Mungu kwa mambo yote aliyokutendea mwaka 2022 maana haikuwa kwa ujanja wako, wala uwezo wako, bali ni kwa neema ya Mungu tu ( 1 Wathesalonike 5: 18- Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu).
4. Omba kibali kwa Mungu cha kuuvuka huu mwaka salama kwa hizi siku chache zilizobaki, usizione ni chache kwa sababu saa yoyote au dakika yoyote au sekunde yoyote linaweza kutokea jambo lolote baya ambalo likasababisha kutoingia kabisa 2023 au ukaingia 2023 bila furaha yoyote. Omba unachokiwaza na kukiongea kikapate kibari mbele za Bwana ( Zaburi 19:14- Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu).
5. Weka Malengo ya mwaka 2023 sasa usisubiri mpaka mwaka ufike ndio uanze kuweka, mwaka ukifika inabaki ni utekelezaji tu wa Malengo uliokwisha yaweka. Pia mkabidhi Mungu hayo Malengo ili shetani asije yakwamisha wakati wa utekelezaji, maana Mungu anasema tumkabidhi njia zetu naye atafanya (Zaburi 37:5- Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya).
6. Ombea mwaka 2023 ukawe wenye Baraka na mafanikio tele, usisubiri mpaka mwaka ufike ndio uanze kuomba hapana shetani atakutangulia. Omba sasa ili hila za adui zishindwe mwaka 2023, mwambie Mungu wema na fadhili zake zikufuate mwaka 2023 kama ilivyoandikwa kwenye Zaburi 23:6 kwamba;- Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele).
7. Vunja roho zote chafu (za mauti,magonjwa,ajali,umasikini, kafara,malipizi,n.k) zinazokufatilia ili zisiingie mwaka 2023. Mwambie Mungu shauri la adui lisisimame kamwe katika maisha yako ila shauri la Mungu ndio lisimame mwaka 2023 kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Zaburi 33:11 kwamba;- Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi).
MPENDWA MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUUSOMA UJUMBE HUU NAAAMINI KUNA KITU UTAKUWA UMEPATA.
NAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2023.
©Msufu-Desemba 30, 2022 mawasiliano 0763242555 na 0753255132

Maoni

  1. Asante Mtumishi kwa ujumbe huu mzuri, hakika Neema na Rehema zake Mungu zinatufanya tuione leo

    JibuFuta
  2. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO # 03: MAAJABU YA NAMBA SABA

SOMO # 01: ADUI

SOMO # 07: MAOMBI